Rapa Ney wa mitego, alipata ajali mbaya ya gari maeneo ya Oysterbay jijini Dar na mguu wake ukashtuka kidogo, ila rafiki yake aliekuwa nae, ameumia kichwani na jana ndio aliruhusiwa kutoka hospitali

Ajali hiyo ilitokea usiku wa juzi kumka jana  maeneo ya mataa ya St Peters, alipokuwa akitokea masaki kuelekea moroko, na  baada ya mataa yake kumruhusu kupita, alikutana na Lori lililokuwa likitokea Mjini kuelekea Moroko pia, likiwa halina taa na kumvaa kwa nyuma na kupelekea gari lake kuingia mtaroni na kuharibika vibaya. Gari alilokuwepo nalo Rapper huyo aina ya  Altezza, ina thamani ya shilingi millioni 14 


Post a Comment

 
Top