Wanafunzi wengi waliomaliza kidato IV mwaka jana sasa hivi wanaweweseka na stori za matokeo kutoka.Upotoshaji umeanzia kwenye page feki za facebook ambayo inaendeshwa na watu wanaojifanya ni Necta, ni page ambazo zimekuwa zikitoa habari za uongo na pia zenye kufanana yani copy na kupaste kitu ambacho kimekuwa kiki wachanganya sana wafunzi waliomaliza pia zimekuwa zikijizolea likes nyingi kila kukicha
 
Kutoka kwa host wa kipindi cha Amplifaya  cha Super brand redio Clouds fm Millard Ayo aliweza kuongea na msemaji wa necta  na kueleza kuwa

 “matokeo ya kidato cha nne hayajatoka bado lakini yakiwa tayari Katibu Mtendaji ataita waandishi na yatawekwa kwenye mtandao wetu wa NECTA, kuna watu wametoa hizo habari kwenye facebook na wanatumia nembo ya baraza la mitihani lakini napenda kukwambia kwamba NECTA hatuna ukurasa wa facebook, hiyo taarifa sio ya ukweli na wala haina uhusiano wowote na baraza la mitihani, matokeo yatatoka kabla ya mwishoni mwa february 2013″

Na hi indo sauti ya mahojiano yao sikiliza hapa 

Post a Comment

 
Top