Mastaa wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kisa kikielezwa kuwa ni mwigizaji , Ruth Suka ‘Mainda’,

Inadaiwa kuwa chanzo cha yote ni pale Steve Nyerere alipoanzisha kampuni ya kazi zake za sanaa akimshirikisha Mainda, jambo linalosemekana kumkera Ray aliyekuwa akifanya kazi na mwigizaji huyo wa kike chini ya Kampuni ya RJ Production.
“Kuna wakati eti Ray huwa hapendi kumuona mtu akiwa karibu na Mainda, mara nyingi huwa anakuwa na wivu kwa kuwa anahisi kuna kitu zaidi ya kazi,” kilisema chanzo kingine na kusisitiza kuwa Ray alimpiga ‘stop’ Mainda kushirikiana na Steve Nyerere huku suala la wivu wa kimapenzi likitajwa.

Ilidaiwa kuwa kabla ya mtafaruku huo, Steve Nyerere na Ray walikuwa ni maswahiba lakini sasa wamegeuka chui na paka na katika kutafuta ‘sosi’ ya yote hayo, ndipo Mainda akatajwa.

Baada ya taarifa hizi kusambaa wasanii hawa walitafutwa alipatikana Steve Nyerere lakin kwa Upande wa Ray alikosekana kwenye simu yake ya kiganjani na pia kwa upande wa mainda simu yake iliita lakin hakupokelewa


Steve Nyerere alisema hivi
“Ni kweli mimi na Ray ni chui na paka lakini sitaweza kukwambia sababu ya ugomvi wetu kwa kuwa nitaibua mambo mengi sana, kipindi hiki nipo katika kubadilisha maisha yangu,”


Post a Comment

 
Top