Msanii anayefanya vizuri kunako gemu ya  muziki wa bongo fleva na filamu pia Hemed Seif Suleiman aka PHD, amesema kuwa mwaka huu hatoigiza sana kwenye filamu za watu kwasababu ameingia mkataba na kampuni moja ya usambazaji ambayo inamtaka kutengeneza filamu zake mwenyewe 7 kwa mwaka.

Hemed alisema kuwa mkataba huo utamfanya yeye kufikiria zaidi filamu zake kuliko kucheza kwenye filamu za watu wengine.

Hemed alieleza kuwa ubize huo wa mwaka pia ndo unamfanya kushindwa kuanza kutengeneza nguo za ndani za wanawake kama alivyosema mwaka huu kuwa anatarajia kuanza kubuni nguo zake za kike za ndani za wanawake.

Alisema kuwa bado mipango ya nguo hizo iko palepale kama ilivyokuwa awali kwa sababu yeye pia ni mbunifu na alikaa chini akafikiria aje na wazo la tofauti.

"Watu kila siku wanajitokeza wanabuni tisheti, makoti na vitu vingine, mimi nilikaa chini nikafikiria kwanini mama zetu, dada zetu wanaenda kununua nguo za ndani za mtumba Mwenge na kwenye masoko mengine?


Nikaona si kitu kizuri kwa kuwa hizo zimetoka nje ya nchi na zimeshavaliwa kwa hiyo mimi ndo nikaona nibuni nguo za ndani kwa ajili yao".

Msanii huyo anasema kuwa ratiba zake za kutengeneza filamu na muziki zitakapokaa vizuri anataka kurudi shule kumalizia shahada yake ya Masoko ambayo alishaanza lakini alishindwa kuendelea kutokana na kazi.

Hemed ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wa 'Going Crazy' anasema baada ya wimbo huo anatarajia kuachia video mbili za nyimbo zake mpya ambazo ni 'Far away' aliyomshirikisha Mabeste' na 'Rest of ma life' aliyomshirikisha Mr Blue.

Post a Comment

 
Top