Msanii wa muziki wa kiazi kipya anayejulikana kama Diamond Platnumz  hivi karibuni alilazimika kuahirisha ziara yake ya barani Ulaya baada ya waandaaji kushindwa kukamilisha malipo yake ya advance katika muda unatakiwa kutokana mna makubaliano.

Kwa habari zilizokuwepo ni kuwa Diamond alitakiwa kulipwa 50,000 USD (Dollar) ambazo ni sawa na shilingi 80 Million za Kitanzania.
Diamond alizidi kufunga kuwa ziara hiyo itafanyika mwezi ujao ambapo baada ya ziara hiyo atarudi nyumbani  Tanzania na kisha kujiandaa  tena kwaajili ya ziara nyingine.

Kutokana na makubaliano mapya ya ziara hiyo kuna uwezekano wa ziara hiyo ya kwanza kumuingizia karibu shilingi milioni 100 ama zaidi.

Jumamosi hii Diamond alilazimika kutumia website yake kutoa taarifa ya kuahirisha kwa ziara hiyo.

“Kutokana na kampuni ya United Events Ltd Tilburg-The Netherlands kwa upande mwingine kama promoter kushindwa kutimiza baadhi ya mahitaji ikiwemo kushindwa kulipa pesa ya show ambayo ilitakiwa ifanyike Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/Germany 09/03/2013 na zingine kama East African Night ambayo ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/Holland tarehe 15/03/2013 na kadhalika, mimi na team yangu nzima ya wasafi hatutoweza kuhudhuria kwenye events hizo,” alisema.

“Nilikuwa nikipata maswali mengi sana toka kwa mashabiki zangu mbalimbali wakiniuliza kuhusiana na ujio wangu wa nchi hizo za EUROPE lakini siku zote nilikua kimya sikuweza kujibu wala kuzungumza chochote na wadau wangu kutokana na kutokuwa na uhakika wa tour hiyo.”

Post a Comment

 
Top