KUINGIA KATIKA SIASA
Baada ya kumaliza masomo alishughulika hasa na biashara
za familia alizorithi kutoka kwa babake.
Kenyatta aliingia katika siasa za Kenya alipoteuliwa kama
mwenyekiti wa tawi la chama cha KANU kilichokuwa kinatawala mwaka 1997. Rais
mstaafu Daniel Moi alimuunga mkono sana na ilitokana na msukumo wake ndipo
Uhuru aliingia katika siasa.
Wengi walitarajia kuwa angeshinda lakini baada ya
kushindwa , Uhuru alighadhabika sana na hata kuahidi kuasi siasa.
Wengi waliona hatua ya Moi kama kumtayarisha Uhuru kwa
mambo makubwa katika siku za baadaye
Mara moja akarejea katika biashara za familia yake ambazo
zinajumuisha hoteli tano mashuhuri, kampuni za vifaa vya ndege na kilimo cha
biashara. Lakini hakujua kuwa Moi bado alikuwa na mpango naye kutaka kumpeleka
katika ngazi za juu.
1999 Rais Daniel arap Moi alimpa cheo cha mwenyekiti wa
bodi ya utalii. Moi aliendelea kumpandisha ngazi kwa kumpa nafasi ya mbunge
mteule na kumfanya waziri msaidizi.
2002 akawa makamu mwenyekiti wa KANU. Chama cha KANU
kuanzai ahpo kikaanza kugawanyika huku vigogo wa chama hicho wakiondoka
chamani.
Tangu alipoingia katika ulingo wa Moi, Uhuru amekwa
akitaka kuonyesha watu kuwa yeye anaweza kujitegmea mwenyewe wala sio kibaraka
cha Moi kama wengi walivyokuwa wanasema. Baadaye alimshinda kigogo wa chama cha
KANU Nicholas Biwot walipogombea uwenyekiti wa chama hicho.
MGOMBEA URAIS 2002
Tangu Julai 2002 ilionekana wazi ya kwamba Moi alimtaka
kama mgombea wa urais upande wa KANU atakayemfuata katika ikulu. Mkutano mkuu
wa KANU katika mwezi wa Oktoba 2002 uliitikia mapenzi ya rais ukamtangaza Uhuru
kama mgombea wa urais.
Tendo hili lilisikitisha wanasiasa wengi wasiokuwa
Wakikuyu na kutegemea nafasi hii kwa ajili yao wenyewe. Waliondoka katika KANU
na kuendelea katika ushirikiano wa upinzani wa NARC.Uhuru ulishindwa katika
uchaguzi wa 2002 alipata asilimia 31 za kura tu.
KIONGOZI WA UPINZANI NA WA CHAMA
Katika bunge jipya alikuwa kiongozi wa upinzani lakini
aliona pia upinzani ndani ya chama hasa kutoka kwa Nicholas Biwott pamoja na
wanasiasa kutoka Bonde la Ufa.
Kwenye mkutano wa chama cha Januari 2005 Uhuru
alithibitishwa kwa kura nyingi na hapo Biwott akodnoka chamani na kuunda chama
chake cha New Kanu.
UPINGAMIZI DHIDI YAKE NDANI YA KANU
Katika kura maalumu ya wananchi kuhusu katiba mpya Uhuru
alishikamana na viongozi wengine katika kambi ya machungwa.
Mipango yake ya kushiriki katika Orange Democratic
Movement(ODM) yalipingwa vikali ndani ya chama kwa sababu wana KANU pamoja na
rais mstaafu Moi waliogopa kupotea kwa chama cha kwanza katika historia ya
Kenya.
Katika Novemba 2006 Biwott alirudia jaribio la kumpindua
Uhuru kwa kuita mkutano wa Kanu mjini Mombasa bila idhini ya mwenyekiti wala
kamati ya chama.
Hapa alichaguliwa kuwa mweyekiti mpya. Kwa msaada wa
serikali Biwott alifaulu kuandikisha kamati yake kama uongozi rasmi hivyo
kumwondoa Uhuru katika nafasi ya kiongozi wa upinzani bungeni.
Uhuru alipinga na mahakama kuu ikabatilisha kura ya
Mombasa tar. 29 Desemba 2006 ikathibitisha azimio hili katika Juni 2007.
KUHAMIA UPANDE WA KIBAKI 2007
Juni 2007 Uhuru alionyesha wazi ya kwamba alitaka kuacha
ushirikiano wa ODM kwa kutopeleka jina lake kati ya wagombea wa urais upande wa
ODM. Badala yake alieleza ya kuwa atampigania rais Kibaki achaguliwe tena.
Alisema hana nia ya kugombea urais ikiwa hana uhakika kuwa atashinda.
Kufuatia uchaguzi uliokumbwa na utata, Kibaki alitawazwa
kama rais licha ya utata huo. Kibaki naye alimteua Uhuru kama waziri wa
serikali za mitaa na baada ya mapataono kati ya Kibaki na Odinga , Uhuru
aliteuliwa kama naibu waziri mkuu ikiwa ni sehemu ya kugawana mamlaka.
Kenyatta ameweza kuchaguliwa kama rais baada ya kumshinda
mpinzani wake Raila Odinga kwa idadi ya kura za urais na kupata asilimia hamini
nukta tatu , kama inavyohitajika na katiba mpya.
Post a Comment