Diva wa filamu za bongo anayejulikana kama Wema Sepetu amemnusuru msanii mwenzake Kajala
Masanja kwenda jela miaka saba baada ya kumlipia faini ya fedha taslimu ya
Sh.milioni 13.
Hata hivyo wakati Kajala akiachiwa huru, mumewe
Faraja Chambo amehukumiwa kifungo cha
miaka 12 jela kutokana na kushindwa kulipa faini ya Sh milioni 213.Mke na mume
hao walihukumiwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu
Mkazi Sundi Fimbo baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatuya kula njama,
kuuza nyumba iliyopatikana katika mazingira ya rushwa ili kuficha ukweli na
kosa la utakatishaji fedha.Mahakama ya Kisutu ilitawaliwa na vituko mbalimbali
kwani wakati hukumu ikisomwa, Kajala alikuwa akilia muda wote hali
iliyosababisha wasanii wengi waliojaa mahakamani kuangua vilio kwa kububujikwa
na machozi kwani hawakuweza kutoa sauti wakihofia kukamatwa kwa kuisumbua
mahakama.Hakimu Fimbo alipomaliza kusoma hukumu Kajala alijikuta akikaa chini
na kulia kwa huzuni, alitolewa nje kuelekea mahabusu na kuwaacha wasanii
wakilia na kupanga jinsi ya kumsaidia aweze kutoka gerezani.
Mama mzazi wa Faraja alitoka mahakamani na kuelekea
katika mahakama nyingine ya wazi, alipofika humo aliangua kilio kikubwa
kilichovuta watu kumfata kujua kulikoni, mama huyo alivua viatu na kuanza
kuwakimbiza wapiga picha walioanza kumpiga picha.
Kuwakimbiza na kuwarushia mkoba wake hakuona kama
inatosha aliamua kuokota mawe na kuwatishia kuwaopiga nayo, walifanikiwa
kumpiga picha lakini walikuja kuondolewa na askari kwa ajili ya utulivu.Wasanii
walianza kuchanga fedha kwa ajili ya kulipa faini ya jumla ya Sh milioni 13
lakini Wema aliwakataza na kuwaambia kwamba fedha zote atazilipa, aliondoka
eneo hilo kuelekea benki na baada ya masaa mawili alirudi na fedha hizo.
Akisoma hukumu, Hakimu Fimbo alisema upande wa amshtaka
katika kesi hiyo ulikuwa na mashahidi saba na waliweza kuthibitisha katika
ushahidi wao kwamba washtakiwa walitenda makosa hayo huku wakijua.
"Kuna makosa matatu, kosa la kwanza wanadaiwa
Aprili, 2010 walikula njama ya kuuza nyumba iliyokuwa Kunduchi Sala sala jijini
Dar es Salaam, Shtaka la pili kuuza nyumba hiyo Aprili 14, 2010 kwa Emiliana
Rwegangira huku wakijua kuna notisi
inayowakata kufanya hivyo na shtaka la tatu la kutakatisha fedha.
"Ili mahakama itoe uamuzi kwa kosa la kula njama
lazima iangalie kosa la pili la kuuza nyumba iliyozuiliwa kuuzwa kwa sababu
ilipatikana katika kwa nia ya rushwa, kwa kuangalia ushahidi mahakama inawatia
hatiani kwa kosa la pili,"alisema Fimbo.Alisema kwa kuwa shtaka la pili
wametiwa hatiani, mahakama inawatia hatiani kwa shtaka la kulanjama kwani
limethibitika. Katika shataka la tatu la kutakatisha fedha, mahakama inamtia
hatiani mshtakiwa Faraja na kumwachia huru Faraja kwa sababu alihusika katika
kuuza nyumba lakini hajui fedha za kujenga nyumba
hiyo zilipatikanaje."Kwa kosa la kwanza la kula
njama, mahakama inawatia hatiani washtakiwa wote na watalipa faini ya Sh
milioni 5 au kwenda jela miaka miwili kama watashindwa kulipa, Shtaka la pili
washtakiwa wote watakwenda jela miaka mitano kama watashindwa kulipa faini ya
Sh milioni 8 na shtaka la tatu faraja anatakiwa kwenda jela miaka mitano
akishindwa kulipa faini ya Sh milioni 200,"alisema.
Baada ya kutoa adhabu hizo wasanii walihaha kuchangishana
lakini Wema aliokoa jahazi kwa kutoa jumla ya Sh milioni 13 kwa ajili ya
kumuokoa Kajala ambaye baada ya saa tatu alifanikiwa kutoa kuelekea
nyumbani.Kajala aliondoka na gari la kifahari eneo la Mahakama ya Kisutu kwa
kulakiwa na ndugu, jamaa na marafiki waliokuwepo eneo hilo.Kajala na mumewe
walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Machi 15, mwaka jana na kusomewa mashitaka
matatu ya kula njama, kubadilisha umiliki wa nyumba baada ya kuiuza na
kutakatisha fedha haramu, kosa ambalo halina dhamana kisheria.
Washitakiwa hao wanadaiwa kula njama ya kuhamisha umiliki
wa nyumba iliyopo Kunduchi, Salasala, Dar es Salaam, kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Pia, wanadaiwa Aprili 14, 2010, walihamisha umiliki wa
nyumba kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.Kajala na mumewe
wanadaiwa katika shitaka la tatu kuwa,
Aprili 14, 2010, wakijua kuwa ni kinyume na sheria, walifanya kosa la
kutakatisha fedha haramu.
Kajala na mumewe wanadaiwa katika shitaka la tatu
kuwa, Aprili 14, 2010, wakijua kuwa ni
kinyume na sheria, walifanya kosa la kutakatisha fedha haramu.
"Hakuna ubishi kwamba washtakiwa walikaa wakaamua
kuuza nyumba, kinachotakiwa kuangalia kama kweli walifanya hivyo kihalali au la
kwani ushahidi ulionyesha washtakiwa wote walishiriki katika utaratibu wa kuuza
nyumba hiyo.
Post a Comment