Jokate Mwanelo ni mtangazaji wa TV, muigizaji wa filamu, mwanamuziki na mjasiriamali. Umaarufu wake ulianza aliposhiriki shidano la Miss Tanzania mwaka 2006 na kukamata nafasi ya pili na kupata ubalozi wa Redd’s na gazeti la The Citizen. Jokate amewahi pia kushinda tuzo za ZIFF kama muigizaji bora wa kike. Pamoja na hivyo hujihusisha na muziki pia ambapo amewahi kushirikishwa na AY kwenye wimbo Kings and Queens na hivi karibuni amesikika kwenye wimbo wa Lucci, Water up.


Leo kupitia The Countdown mabyo huruka kuanzia saa tisa mchana hadi za 11 jioni. Ni kipindi cha kila wiki ambacho huwa na mkusanyiko wa nyimbo 20 bora zilizochaguliwa kwa mapenzi yake mtu maarufu kwenye maeneo mbalimbali husasan katika tasnia ya burudani.

The Countdown hucheza nyimbo 20 zilizochaguliwa na mtangazaji wa wiki husika. Nyimbo hizo huzichagua mwenyewe kulingana na muziki anaopenda kuusikiliza kila siku. Hizo huwa ni nyimbo zinazotafsiri wajihi wao pamoja na nyimbo ambazo ziliwasaidia katika vipindi mbalimbali vya maisha yao.

Hivi karibuni alijiingiza kwenye biashara ya ubunifu wa mitindo kwa kuanzisha kampuni na brand ya Kidoti ambayo hubuni nguo pamoja na kutengeneza nywele za aina mbambali zinazopatikana nchini.


Post a Comment

 
Top