ARTIST: NEY WAMITEGO FT DIAMOND
PRODUCER: MR TOUCH
CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney)  X2

DIAMOND

Hata bibi yangu mi aliniambia , mwanamke anahitaji kubembelezwa
Kupetipeti matunzo pia, ukienda rafu utampoteza,
Muziki ni mfano wa binti muzuri,
Na ndio maana namtunza kwa   vazi na uturi

NEY WA MITEG

Aaah piga kimya, we ndo haufai kabisa hauna maana
Wabana pua kila siku mnarogana, bibi yako alikuambia muziki ni kama binti
Mbona unawachezea unawatema kama big g
Mara wema, mara Jo keti, mara Naj, mara Penny, je mnafanya mziki mpate mabinti

DIAMOND

Uuuhhuuuu, hata wazee wazamani, walishasemaga kazi na dawa
Chamuhimu jukwaani, ni kuhakikisha wanapagawa,
Kwa michezo ya kuringa ringa  ndo huwa wanadata
Badilika usiwe mjinga, utawakamata

CHORUS

Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).
Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney)  X2
 
NEY WA MITEGO

Muziki wenu ushirikina ndio umetawala, q chilla analalama anasema umemroga
 Mganga wako aliekutoa umemkimbia hujalipa,  bila skendo za magazeti basi huskiki

DIAMOND

Mi ni mti wenye matunda, milele siogopi kupigwa mawe
Ubaya wenu wengi kayumba, elimu mliitupa sandakalawe

NEY WA MITEGO

Bado hujanishawishi, bongo fleva inanipa kichefu chefu
Kwanza nyie malimbukeni wa umaarufu
Mnalenta maringo mpaka kwa mashabiki , Wabana pua nyie watoto sio riziki,
Mnavaa nguo za dada zenu, zinawabana mapaja nyie makaka duu
Aah nyie watoto mchele mchele , kwenye show viuno mbele mbele X2
Nimewanyamazisha, brazameni vipi  we bado unabisha


DIAMOND

Mi nnamengi nnayajua, ila we ni mtemi utaanzisha utata
Michezo yenu kutoboa pua, bora ninyamaze usinipige mbata

Post a Comment

 
Top