Imetokea leo hii dakika chache zilizopita Morogoro Road na Indira Gandhi (City Centre - Dar), Inasemekana Watu wapatao 60 walikuwepo ndani yake.. watoto wa Madrassa walikuwemo katika jengo hili na pia mpaka sasa maiti zilizoopolewa ni 14 na majeruhi zaidi ya 30 wamekimbizwa hospitali, Bado pia kuna baadhi ya watu hai ndani yake.

Jitihada za uokoaji zimeanza kufanyika, Waziri Nchimbi tayari amekwishafika eneo la tukio mpaka sasa japo kuna uhaba wa vyombo vinavyostahili kushughulikia hali hii.





Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, jengo lenye ghorofa 14 jijini Dar es Salaam limeanguka na kusababisha vifo vya makumi ya watu.

7966_10151611586205649_2055408267_n

“Kuna jengo la ghorofa 14 lililokuwa bado linajengwa mtaa wa Indragandhi/Morogoro limeanguka. Limeangukia uwanja wa michezo wa Msikiti wa Shia Ithna Asheri upande wa mashariki. Inasadikika watoto waliokuwa wanacheza kwenye uwanja wa michezo na wafanyakazi wa ujenzi wamefukiwa. Kwa sasa tunaendelea na jitihada za uokozi na tutatoa taarifa baadae.”

Picha ya jengo hilo baada ya kuanguka

Picha ya jengo hilo baada ya kuanguka

IMG-20130329-WA001

BBC Swahili: Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada.

“nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia mayowe,” alisema shahidi mmoja.Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na lilianguka saa tatu kasorobo asubuhi kwa saa za afrika mashariki. Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado haujulikani.

Nayo website ya Global Publisher imeandika: Taarifa zilizotufikia ni kwamba jengo lenye ghorofa 16 lililokuwa bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indira Gandhi na Morogoro jirani na Burhani limeanguka. Inasemekana katika jengo hilo kulikuwa na watu takribani 60 ambao wanahofia kupoteza maisha.

8041_507400472651585_1574623982_n

578200_395382197227217_659029494_n

Post a Comment

 
Top