Msanii anayefanya vizuri kwenye upande wa bongo Saimon Mwapagata almarufu kama ‘Rado’ amenusurika kifo kutoka kwa vijana waliofunga njia maeneo ya Mwananyamala, jijini Dar Jumapili iliyopita.
Taarifa kutoka kwa  rafiki wa karibu wa Rado ambaye pia naye msanii wa filamu, Deogratius Shija, tukio hilo lilitokea usiku wakati Rado alipokuwa akirudi nyumbani kwake
“Alikuta njia imefungwa na vijana watatu, alijaribu kuwapigia honi lakini hawakufungua njia.
“Rado alishuka kwenye gari na kuwauliza kwa nini wamefunga njia wakamjibu kwamba mmoja wao ameibiwa simu, hivyo wanamtafuta mwizi wao.
Shija aliongeza  kuwa vijana hao walimvamia Rado  na kuanza kumpiga  kwa  mapanga na marungu na kusababisha rado kupoteza fahamu.
 Shija alizidi kuongeza na kusema “Nilipigiwa simu na msamaria  na kuambiwa kuwa Rado hajiwezi, sababu kuna watu wanaomjua maeneo yale alipelekwa Oysterbay Polisi kisha kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala ambako alishonwa, kifuani na mguuni,”

Post a Comment

 
Top