Diamond na Uwoya, walifanya jitihada za hali ya juu
kuuficha ukweli kuhusu uhusiano wao lakini ilipofika Machi 25, mwaka huu,
walinaswa kwenye hoteli moja yenye hadhi ya nyota tano, iliyopo Mbezi Beach,
Dar es Salaam.
Ijumaa lina ushahidi wa kutosha kutamka kwamba
Diamond na Uwoya, walilala kwenye hoteli hiyo, chumba namba 208, waliingia saa
8:24 usiku kisha wakatoka kati ya saa 9:00 na saa 9:13 mchana.
Hii ni skendo
inayoweza kuweka rekodi ya kukaa kwenye vichwa vya watu kwa muda mrefu
ujao, kwani Uwoya siyo tu kwamba ni mke wa mtu, bali pia ni juzijuzi tu
alijidai amesahihisha makosa yake kisha akathibitisha kurudiana na mume wake,
Hamad Ndikumana ‘Kataut’, baada ya kutengana kwa kitambo kirefu kidogo.
Skendo hiyo, inakuja na picha yenye mshtuko mkubwa kuhusu
Diamond ‘Sukari ya Warembo’, kwani baada ya kumpitia Uwoya, ni dhahiri kwamba
ndani ya Klabu ya Bongo Movie amebakiza wa kuhesabu, tena ni wale ambao mvuto
wao ni wa kumulika kwa tochi, vinginevyo, vinara wote ameshadondoka nao
dhambini.
Kwa kuanzia na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Jokate
Mwegelo, Aunt Ezekiel, Uwoya ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo
Movie Unit pamoja na warembo wengine kibao, ni wazi sasa mtandao wa ngono wa
Diamond, unagusa karibu asilimia 97 ya mastaa wote wa filamu na muziki
nchini...
Post a Comment