David-Banda-Goes-Tour-Madonna



Rais wa Malawi, Joyce Banda amechukizwa na kitendo cha  mwanamuziki Madonna baada kusema kuwa atajenga shule kujenga shule 10 zenye thamani ya paundi million 10 nchini humo lakin badala yake mpaka sasa hajajenga shule hata moja.Madonna alianzisha mradi wa Raising Malawi baada ya kuudopt(kuchukua mtoto amabe hajamzae nchini Malawi) mtoto wake wa kiume David Banda mwaka 2006 na mtoto wa kike Mercy James mwaka 2009 nchini humo.

Rais  huyu  anazidi kungeza kuwa  mwanamuziki huyo hakutimiza ahadi yake ya kujenga shule ya wasichana kwa paundi milioni 10 na badala yake kuamua kujenga shule 10 bila kuwataarifu maofisa.

Alisema: “Ziko wapi hizi shule 10 alizojenga?

“Sehemu zingine alikarabati tu majengo yaliyopo tayari. Hakuna mtu anayetakiwa kuja hapa na kusema, ‘najenga madarasa bila kukaguliwa.
“Ni tusi kwa watu.”


Post a Comment

 
Top