P-Square jet
Kufuatia uvumi kuwa P Square wanamiliki Private Jet wakali hao wameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia tetesi hizo wakikanusha kuwa si kweli.
P Square wamesema kwamba kilichopo nimakubaliano na kampuni fulani ya Private Jet kutumia ndege hiyo kwenye safari zao kwasababu inarahisisha mambo mengi.
Hata hivyo wakali hao wamefafanua kuwa kukodi private Jet hakuna maana kuwa hawana uwezo wa kununua ya kwao kwasababu hata sasa wanapanga kununua Jet yao binafsi maalumu kwa safari zao.

Aidha Wakali hao wameongela kusikitishwa kwao baada ya kusikia habari za kufungiwa kwa single yao ya Alingo.
“Tumeskia kuhusu kukatazwa wimbo wa Alingo, lakini hatujapewa sababu za msingi kwanini imefikia hatua hiyo. Tulichogundua ambacho hawajui ni kwamba unapoufungia wimbo unaufanya upate umaarufu haraka, na kukataza wimbo kwenye channel Nigeria si jambo la msingi kwasababu channel za kimataifa wanaendelea kuupiga”. Alisema Peter
CHANZO BAABKUBWA

Post a Comment

 
Top