Ramani ya muonekano wa ndani
Ramani ya muonekano wa ndani
Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) April 4 2013 imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.
Website ya Yanga (youngafricans.co.tz) imeandika kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.
kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.
Ramani ya muonekano wa nje wa Uwanja huu mpya wa Yanga uitwao Kaunda.
Ramani ya muonekano wa nje wa Uwanja huu mpya wa Yanga uitwao Kaunda.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wamepewa nafasi kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba kwa ajili ya ujenzi. 
Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga ambapo kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga, ujenzi unaotarajiwa kuanza July 2013 utachukua muda wa miaka miwili kukamilika.
Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.

Post a Comment

 
Top