Staa wa Bongo Movie ambaye pia ni mmilikiwa kampuni ya Endless film  Wema Sepetu amemfikisha mama yake mzazi anayejulikana kama Miriam Sepetu kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama jijini  Dar es salaam kwa madai ya kwenda nyumbani kwake na kufanya vurugu zilizosababisha kuharibika kwa samani nadani ya nyumba yake.

Tukio hilo lilitokea  usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, jijini Dar.

Mbali na mama mtu, wengine waliofikishwa kituoni hapo ni dada mkubwa wa Wema aitwaye Nuru na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Bestizo ambaye inasemekana ni mshirika mkubwa wa Diamond kwenye masuala ya mtandao wa msanii huyo.

“Wema alikuwa nyumbani kwake usiku huo, watuhumiwa hao wakamzukia na kuanza kumchapa makofi ya ‘kelbu’ ambapo katika mshikemshike huo, baadhi ya vitu vilivunjika na kumtia hasara staa huyo,”
Haikujulikana mara moja ni kitu gani kilisababisha mama mzazi huyo, dada mtu na kijana asiyekuwa ndugu kwenda kwa Wema na kutenda kosa hilo.

Wema alikwenda polisi na kuandikisha maelezo ambayo yameingizwa kwenye jalada lenye kumbukumbu; KJN/RB/2755/2013 SHAMBULIO, KUHARIBU MALI.

Post a Comment

 
Top