Staa wa filamu za Kibongo anayefanya vizuri sana anaye julikanaka kama  Yusuph Mlela amedaiwa kumpa  ujazito mwanafunzi wa chuo cha ITF kilichopo Tandika, jijini Dar amabpo mwanafunzi huyo ni mwenyeji wa zanzbar aliyefahamika kwa  jina moja la Salha.
Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi  huyo kwa muda mrefu ambapo marafiki wote wa Salha, walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa ujazto huo kasha kuukataa na kusema hataki mtoto.
Hii ni kauli ya mwanafunzi mwenzie na salha amabye alikuwa anajua uhusiano kati ya salha na Staa wa bongo movie Yusph mlela
 “Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema hahitaji mtoto, atoe mimba.

“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’
Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na kusema hamtambui na wala chuo  anachosoma hakijui.

“Huyo msichana simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko,  kama huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.

Post a Comment

 
Top