Mchekeshaji mahiri hapa Bongo  anayejulikana kwa jina la Masanja Mkandamizaji kutoka kwenye moja ya mitandao hapa bongo imeandika kuhusu utajiri wake pamoja na mali na magari sita ikiwamo Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa anayomiliki ikiwepo kampuni ya Ulinzi pamoja na mashamba yaliyomo kigamboni lakin kubwa zaidi ni lile la Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.Haikuishia hapo tu aidha msanii huyu anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.
Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.

Credit Globalpublisher

Post a Comment

 
Top