Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alishawahi kuwika katiaka shindano la Tusker Project fame anayejulikana kama Peter Msechu akiwa na
muonekano mpya kabisa kwa mwaka 2013, ameendelea kufanya yake katika muziki
akiwa na mzigo mpya kabisa kwaajili ya wale wanaopenda kazi zake ambapo kwa
habari zilizoko sasa ni kwamba kuna ngoma ambayo ameifanya na Producer Fundi Samweli wakati bado yupo
hapa Bongo, na mixing yake imefanyika huko Marekani, kazi ambayo ndiyo
atakayofungua nayo mwaka.
Msanii huyu ambaye kwa sasa ameamua kunyoa nywele zake
zilizokuwa katika mtindo wa rasta, pia amepata nafasi ya kuongea na eNewz
kuhusiana na muonekano wake huu mpya huku akisema ni maamuzi tu pamoja na
maombi ya mashabiki wake wengi ndiyo yaliyompelekea kunyoa rasta.
Msechu pia amekiri kuwa Rasta zilikuwa zikimzingua wakati
mwingine na kwa sasa anafurahia mtindo wake mpya wa nywele fupi, wito wake
mkubwa kwa mashabiki ukiwa ni kusuburia ngoma yake hii mpya ambayo ndani yake
amemshirikisha rapa Joh Makini.
Post a Comment