Msafara wa Rais
waua trafiki mchana
huu...
...............Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi
tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari
zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.
Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:
Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so
akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua kwenye spidi kali
sana. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from
Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa
ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna
magari yanayo-cross from Shekilango.
Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua
upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa
madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua
tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa,
ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona
nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na
wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri
kutazama.
BWANA AMETWAA BWANA AMETOA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Post a Comment