Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayejulikana kama Queen wa bongo Fleva Judith Wambura ‘Lady JayDee’ kuonekana kutuma ‘Tweets’ zilizobeba mafumbo huku akitoa mazito ya moyoni juu ya mtu
anayemvurugia mipango yake ya kimuziki hakuweza kumtaja jina mume wake Gadna Habash afunguka juu ya
‘Tweets’ hizo
Akizungumza jijini Dar es Salaam hili hivi karibuni Gadna
alisema kuwa ‘tweets’ alizoziweka msanii huyo zinalenga kufikisha ujumbe
alioukusudia hususani kwa baadhi ya watu wanaomuwekea mipango mibaya ya
kuharibu kazi zake za kimuziki
Alisema kuwa wapo baadhi ya washika dau wanaojikita
katika maswala ya muziki kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku wakimnyonya
mwanamuziki bila ya kujali jasho lake na nguvu yake kwa kazi anayoifanya
Kutokana na hali ya kunyonywa wasanii na washika dau hao
alisema msanii atakapopata akili na kuwa na uwezo wa kugundua kuwa ananyonya na
hawezi kufika mbali hali inabadilika kwa kuanza kukandamizwa na kuwekewa
vikwazo katika kazi zao
“Baadhi ya washika dau wanawaogopa wasanii wakubwa kwa
kuwa tishio katika biashara zao hivyo hata wasanii wachanga pia wananyimwa
nafasi ya kukua kisanii kwa kuhofia kuja kuwageuka baadaye pindi watakapopata
nafasi ya kufanya hilo” alisema Gadna
Aliongezea kuwa mfumo wa muziki hauko sawa na upo kwa
lengo la kumnyonya msanii hali ambayo inazidi kudidimiza wasanii na muziki wa
nchi hii hali inayosababisha muziki unakuwa kwa kusikilizwa redioni na si kwa
kukuwa kwa kipato kwa wasanii
Alisema kuna hujuma zinazoendelea kwenye soko la muziki
zenye lengo la kumnyonya mwanamuziki na kumpa utajili mdau wa muziki sababu
hiyo inapelekeea wanamuziki wa nchi yetu kutoendelea katika soko la muziki
Lady JayDee hivi karibuni amekuwa akitumia mtandao wa
Twitter kwa ajili ya kutuma ’tweets’
zenye ujumbe kwa mtu aliyemkusudia ingawa hazikuonyesha wazi wala kutaja jina
la muhusaka
Hizi ni baadhi ya ‘tweets’ zilizotumwa na msanii huyo
Lady JayDee ?@JideJaydee
Hata nyimbo zisipopigwa now mi sio underground, won’t
complain. Nani asiemjua JayDEe? Am not crazy
Lady JayDee ?@JideJaydee
Basi mjue kuwa tatizo langu sio nyimbo kutopigwa redioni.
Its more than that. U dig??
Lady JayDee ?@JideJaydee
Now nategemea nguvu ya uma #diehardfans
Lady JayDee ?@JideJaydee
Na tweet hivi sbb sikuwahi kulalamika nikaamua kufanya
kazi. Lakini kazi inapowekewa uzito wa jiwe isipenye. That’s another case (22)
Post a Comment