Hivi karibuni nilikuletea story ya Aboubakar Katwila
kujiachia na staa wa muziki na filamu za Kibongo anayejulikana kama Zuwena
Mohamed ‘Shilole’ hivi sasa shilole amenaswa na bwana Mzungu aliyetajwa kwa jina moja la
George.
Ilidaiwa kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara ya shoo,
Shilole hakuondoka jijini hapa na badala yake alionekana sehemu tofauti
akijivinjari na jamaa huyo ambaye uchunguzi wetu ulibaini kuwa ni bosi wa klabu
moja maarufu ya usiku Kanda ya Ziwa.
Kabla ya kuondoka katika jiji hili la sangara na sato,
Alhamisi iliyopita na ndege ya jioni, Shilole alinaswa kimalavidavi na Mtasha
huyo Jumatano katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere wa Gold Crest kulipokuwa na
maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Syria.
Shilole alishuhudiwa akifanyiwa ‘shopping’ ya kufuru na
bwana huyo ambapo gazeti hili lilinasa mpango mzima ambapo lilipotaka kujua
kama ni wapenzi, Mtasha huyo alijibu kwa kifupi sana: “No comment” (sina la
kusema).
Kwa upande wake Shilole alipobanwa mbavu alifunguka: “Nisingependa
kuongelea jambo hilo kwani sasa najipanga kimuziki zaidi, shopping ni mambo ya
kawaida sana kwa hiyo ni vyema tukaongelea muziki wangu kwani shoo yangu ya
Pasaka ilijaa mashabiki wa kufa mtu so nakubalika sana Mwanza na siku moja
nitaweka makazi hapa.”
Post a Comment