Sheha
Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa
katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh
Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo
kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio
na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua
aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha
Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja
akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi
Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.
Post a Comment