EDITOR WA PICHA HII ALISAHAU KUKATA VIZURI NA KUONDOA BACKGROUND NYEUPE KWENYE ENEO LA NYWELE LILILOZUNGUSHIWA DUARA
Kuna habari tumeletewa na msomaji wa tovuti yetu ya bongo movies kumhusu mwanadada wetu muigizaji wa Filamu aliyepata tuzo hivi karibuni, Jennifer Kyaka al-maarufu kama Odama kuhusu safari zake za kwenda nje ya nchi.
Habari au tuhuma hizi tuziite, zinasema kuwa mwanadada huyo huwa haendi nje ya nchi kama anavyowaambia fans wake kupitia blog yake ya odama1.blogspot.com kuwa anasafiri kwenda nje kikazi zaidi, na badala yake inasememekana eti huwa anabaki hapa hapa nchini akizuga yupo nje ya nchi lengo ni kutafuta “KIKI” ama umaarufu kama watoto wa mjini wanavyosema.
Mdau aliyetutumia habari hizi amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha na katutumia picha mbalimbali toka kwenye mtandao mmoja wa kijamii ambako staa huyo yupo zikimuonesha akiwa maeneo mbalimbali ya “duniani huko” ambayo kwa kuangalia picha hizo anasema kuwa ni feki na zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia tuu ya ku-“edit” picha maarufu kama “PHOTOSHOP”
Swali ni je, hili suala ni la kweli? Tunaomba wadau wenye majibu na utaalamu wa picha watusaidie kwa kutazama picha hizi na kutuambia kama habari hii ina ukweli wowote.
Habari kwa hisani ya Teddy Kibs
CHANZO : BONGOMOVIES.COM
ANGALIA UBORA WA PICHA YA ODAMA NI TOFAUTI KABISA NA UBORA WA PICHA YA BACKGROUND ILIYO NA MAGOROFA. PIA ANGALIA HILO BOMBA LILITAKIWA LIONEKANE VIZURI KWA SABABU LIPO KARIBU NA CAMERA LAKINI HAIKUA HIVYO. KOSA LA PILI LA EDITOR
KATIKA PICHA HII EDITOR KAKOSEA KULETA UHALISIA HAPO ODAMA KAWA MREFU SANA
Post a Comment