Mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wameungana na Familia ya Mchungaji, Habakuki Lwendo na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika mazishi ya Binti yao Wende Lwendo aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Uhandisi Kompyuta katika mazishi yaliyofanyika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wende alifariki Ijumaa ya Julai 12, 2013 wakati akijumuika na rafiki zake kuogelea Bahari ya Hindi eneo la Ufukwe wa Kipepeo Kigamboni kilometa chache kutoka eneo alilokuwa akishi.
Mazishi hayo mbali na wanafamilia na wanafunzi wa IFM kuhudhuria pia yalihudhuriwa na Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania, Askofu, Dk Alex Malasusa, Makamu Mkuu wa Chuo cha Tumaini Makumira, Prof. Parsalaw pamoja na wachungaji mbalimbali na Wafanyakazi wa Chuo cha Makumira anakofanyia kazi Mchungaji, Habakuki Lwendo ambaye ni baba wa Marehemu Wende.
 

Post a Comment

 
Top