Nape Nnauye ameamua  kuvunja  ukimya  na  kutoa  utetezi  wake  kuhusu  kauli  yake chafu  iliyochapishwa  na  gazeti  la  Mtanzania  likimtuhumu  kuwatusi  wazee  waliopendekeza  uwepo  wa  serikali  tatu.....

Huu  ni  utetezi  wake:

"Nimestushwa sana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwakweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikuwa ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wana wajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wana wajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!

Imenisikitisha  sana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity"

Post a Comment

 
Top