Leo
tarehe 15 Julai, 2013 majira ya mchana, mwenyekiti wa chama cha CHADEMA
Mhe. Freeman Mbowe amejisalimisha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,
kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikimkabili zikiwemo kauli za
uchochezi ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Jeshi la Polisi, Vyombo
Vingine vya dola na Serikali kwa ujumla.
Jeshi
la Polisi nchini, linaendelea kumhoji Mhe. Mbowe juu ya kauli hizo
ambazo zimekuwa na mlengo wa uchochezi na kuijengea jamii taswira hasi
juu ya vyombo vya ulinzi na usalama na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.
Aidha,
uchunguzi wa kina unaendelea na pindi itakapothibitika kuhusika kwake
ama mtu mwingine yeyote kutoka ndani au nje ya chama cha CHADEMA hatua
zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Post a Comment