Ommy Dimpoz ashirikishwa na DJ maarufu wa Afrika Kusini, Oskido





Ommy Dimpoz ameendelea na mikakati yake ya kujiimarisha zaidi nje ya Tanzania na hivi karibuni alipohudhuria tuzo za CHOAMVA 2013 jijini Johannesburg, Afrika Kusini alitumia fursa hiyo kutengeneza contacts na wadau muhimu kwenye muziki wa Afrika.

Miongoni mwa watu muhimu aliokutana nao na kuzungumza biashara ni DJ na mshindi wa tuzo wa Afrika Kusini DJ Oskido. Si kukutana tu, DJ huyo amemshirikisha Ommy Dimpoz kwenye wimbo wake.

“Legendary feat Upcoming Oskido Feat OmmY Dimpoz South meet East.... Thank ALLAH.....levels,” Ommy ameandika kwenye video aliyopost kwenye Instagram inayomuonesha akiwa studio na DJ huyo.

Awali Ommy alipost picha akiwa na nguli huyo wa muziki wa house na kwait nchini Afrika Kusini nyumbani kwake na kuandika:

“With the Legendary OSKIDO @oskidoibelieve at his Crib #Business.”

Oskido ni DJ anayeheshimika sana nchini Afrika Kusini na kazi hii ikitoka itamsaidia Ommy Dimpoz kuongeza umaarufu wa jina lake barani Afrika.

Post a Comment

 
Top