Msanii Shetta anayefanya vizuri kwenye mziki wa bongofleva amepata ajali ya gari maeneo ya Minjingu akielekea Babati kwa ajili ya kufanya show ambayo maamuzi ya kuifanya yalikuja dakika za mwisho. Wakiwahi show kwa kutumia usafiri wa gari aina ya Noah, walipata hiyo ajali jioni ya April 11 2014 baada ya gari kupinduka wakati dereva akiwa kwenye jitihada za kumkwepa Punda.
Kwenye gari hilo, Shetta alikua na Msaidizi wake pamoja na Waandaaji wa show ambapo hakuna aliepoteza maisha isipokua majeraha madogomadogo huku yeye mwenyewe akiumia kichwani na mguuni.
Shetta alipelekwa hospitali lakini baadae aliruhusiwa kuondoka na kuendelea na safari japo haijajulikana kama aliweza kufanya hiyo show baada ya kugundua kwamba alikua ameumia kidogo.
Hii picha hapa juu ni ya Shetta kwenye eneo la ajali muda mfupi tu baada ya kutokea ambapo baadae aliandika
‘nashukuru Mungu nimetoka salama, kweli Mungu mkubwa maana nilijua leo ndio mwisho wangu, ajali ni mbayaa sanaaaa, thanks wote mlionipa pole tupo pamoja’.
Credit Millardayo.com
Post a Comment