Michuano
ya kombe la dunia imeendelea kuonyesha ukubwa wake kwa kuteka kila
habari kuu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mabilioni ya
watu duniani kote wakiwemo mastaa wakubwa wa kitaifa na kimataifa
wanafuatilia michuano hii ambayo ndio mikubwa kabisa katika soka
duniani.
Mmoja
wa mastaa wa kibongo ambaye ameonyesha kufuatilia michuano hii pamoja
na wachezaji shiriki ni Jokate Mwegelo, ambaye mtangazaji wa TV,
muigizaji na mmiliki wa lebo mavazi na fashion kiujumla ya Kidoti.
Tangu
kuanza kwa michuano hiyo Jokate amekuwa akiposti posti tofauti
kuhusiana na michuano hiyo, huku akionyesha namna anavyomkubali
mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Real Madrid
na timu ya taifa ya Ureno inayoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu.
“Ronaldo
ni mchezaji mzuri, anajituma uwanjani na anafunga magoli akiisadia timu
anazochezea. Ana nidhamu ya kazi yake na akiifanya anaifanya kiuhakika
na ndio maana tangu akiwa Manchester United nikajikuta namshabikia.
Pamoja na hayo kitu kingine ambacho kinanifanya kumkubali Ronnie, ni
namna ambavyo anajitoa kusaidia watu wasiojiweza, kama tulivyosikia juzi
ametoa kiasi cha zaidi ya millioni 100 za kitanzania kusaidia matibabu
ya mtoto aliyekuwa na matatizo fuvu la ubongo kujaa damu.”
Akizungumzia
michuano ya kombe la dunia, Kidoti alisema, “Kwenye michuano hii
nilikuwa nasapoti timu za Afrika lakini zinaniangusha, hazichezi vizuri.
Pia naisapoti Ureno kwa sababu ya nampenda Ronaldo, na Brazil pia
nawapenda wanacheza vizuri hasa yule Neymar. Van Persie pia namkubali,
lile goli alilofunga dhidi ya Spain kwa kichwa, aisee ni moja ya magoli
bora kabisa.”
Post a Comment