Diamond Platnumz


Msanii Diamond Platinumz kwa sasa ndiye msanii kutoka Tanzania anaelipwa pesa nzuri zaidi kwa show zake za ndani ambazo zinakaribia kugarimu milioni 10 au 8 zikiwa ni pesa za kitanzania a,bazo huapata kwenye show moja


Kwa mujibu wa maneja wake ambaye ni Babu Tale anasema hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania).

“Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.” Babu Tale aliiambia Bongo5.

Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani).

“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya.

Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500).
Credit bongoclantz.com

Post a Comment

 
Top