Tukiwa tunaelekea mwisho wa mwaka wasanii wengi wa Bongo wanaendelea kuachia karata zao za mwisho za kufungia mwaka.
Vanessa - coming soon
Vanessa Mdee ni miongoni mwao, kwani anatarajia kutambulisha kazi yake mpya Jumanne Nov.18.
vanessa2
Wimbo wake mpya unaitwa ‘Siri’ akiwa ameshirikiana na Barnaba. Kwenye cover ya wimbo huo kukiwa na mstari usemao “Kwanza ningekuomba kipenzi ukubali tutafanya siri ya watu wawili”.
Kala coming soon
Msanii mwingine anayetarajia kuachia wimbo mpya hivi karibuni na rapper Kala Jeremiah, wimbo wake unaitwa Usikate tamaa akiwa amemshirikisha msanii wa R&B wa muda mrefu Nuruwell, msanii ambaye miaka michache iliyopita alipotea kwenye bongo fleva.
Kala ameiambia Bongo5 kuwa bado hana tarehe kamili ya lini wimbo wake utatoka kwasababu bado kuna mambo anayakamilisha, lakini utatoka siku si nyingi.

Post a Comment

 
Top