Wakati mwanamziki wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz akiendelea kupepesa macho na kutikisa masikio kukanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwingizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ukaribu wao bado unatia mashaka na kuendeleza sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wapambe wao.
Japo kuwa Ommy alielezakuwa yeye na Wema ni marafiki toka kitambo kabla hata ya wema kuwa na mahusiano na mwanamziki Diamond, lakini hii imezidiii.
Mbali na kuonekana wawili hawa kuwa pamoja sehemu mablimbali za starehe toka Ommy atoke Marekani, hili la kupikiwa na kupakuliwa nyumbani kwa Wema ndio limezidi kuchochea hisia kuwa wawili hao wanamahusiano zaidi ya USHKAJI.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram mwanadada Wema ambae na folloers zaidi ya laki nne , alibandika picha hiyo hapo juu akionekana kumpakulia chakula ambacho alijisifia ni kizuri na amekipika mwenyewe na kumtania Ommy kuwa alikuwa analeta pozi kwenye kula.
“Dat moment anapokuja home and umepika chakula alafu analeta pozi at first then unashangaa anaenda sahani mbili.... Talk About Good Food Made Real Good”- Wema aliandika mara baada ya kutupia picha hiyo.
Japo kuwa hadi sasa mwanadada Wema Sepetu ajajitokeza kukataa au kukubali juu ya yeye kuwa na mahusiano na Ommy lakini idadi kubwa ya wampambe wake mitandaoni na ifagilia sana hii “Couple”.
Tuvute subraaa.
Mzee wa Ubuyu
Post a Comment