150204101142-07-transasia-0204-super-169
Mtoto wa kiume wa miaka miwili ni mmoja ya watu walionusurika kufariki katika ajali ya ndege ya TransAsia iliyoua watu 31 huko Taiwani baada ya kukosa mwelekeo na kuanguka mtoni katika mji wa Taipei.
Mpaka sasa tayari watu 15 wameokolewa ikiwemo watoto wengine wanne ambao umri wao haujatajwa huku watu wengine 12 hawajulikani walipo.
tod
Waokoaji wakimchukua mtoto huyo baada ya kumwokoa kutoka kwenye ndege hiyo
Mtoto huyo alikutwa akilia nje ya ndege hiyo na kuchukuliwa na waokoaji kisha kumkimbiza hospitali.
todl
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 58 ilipita karibu na magari na kudondoka mtoni muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan, Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan huku  chanzo cha ajali  kikiwa bado hakijajulikana.

Post a Comment

 
Top