nay wa mitego na mtoto wake



Baada ya Story kuzagaa juu ya uhalali wa mtoto wa Msanii wa Bongo Fleva, Hit Maker wa Single ya Akadumba Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ambaye alizaa na Siwema Edson, taarifa za majibu ya DNA kuhusu damu ya mtoto huyo ni ya Ney ama lah na majibu ya mtoto Curtis ni mtoto halali wa Nay wa Mitego.

Nay na Siwema waligombana baada ya Nay wa Mitego kumfumania Siwema na baadae Siwema kudai kuwa Nay wa Mitego hajazaa naye..

“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.

“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi tena.

“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.

Na sasa kwa Taarifa zilizopo Nay Wamitego yupo ametapa kifaa kipya kutoka Bongo Movie na anajulikana kwa Shamsa Ford.

Post a Comment

 
Top