Kikao cha Bunge kimevunjika leo asubuhi baada ya kutokea vurugu za maneno kufuatia wapinzani kutaka Waziri Mkuu atoe taarifa juu ya mwenendo wa kura ya maoni ya katiba mpya April 30,2015.
Kutokana na vurugu hizo za dakika kama 10 hivi Spika Anna Makinda alisitisha ghafla shughuli za bunge hadi mchana.
Hali likuwa hivi:
Mnyika: Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima.
Mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na lilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie.Tunaomba majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano.
Spika Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza( Hoja ya mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ambaye alipendekeza kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa isogezwe mbele na badala yake kuwe na katiba ya mpito kuelekea uchaguzi mkuu)
Baada ya kauli hiyo, Mnyika na wabunge wa upinzani walianza kupiga kelele bungeni wakidai kuonewa huku wakimtuhumu Spika Makinda kuibeba serikali.
Hata hivyo, Spika hakuonesha kutishwa na kelele hizo na badala yake alimtaka katibu wa Bunge atoe mwongozo wa kile kinachofuata.
Katibu alisimama na kuanza kusoma miswada ya habari ambapo wapinzani nao walisimama na kuzidisha kelele huku wakisema:"Tunataka majibu..Tunataka majibu. Tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali.??!!!
Hali hiyo ikamlazima Spika Makinda Kuliahirisha Bunge hadi mchana.
Tazama Video hapa
Post a Comment