Ndoa yangu ilifikia ukingoni rasmi mwaka Juzi 2013 mwezi Februari, hata hivyo kabla ya hapo tulikua tumetengana kwa karibu mwaka mmoja nyuma.

Chanzo cha ugomvi wetu ni usaliti aliokua akiufanya na dogo mmoja Dalali wa magari. Zilikua ni tuhuma tu ila baadae zilikuja kuwa taarifa za kweli walipotaka kufunga ndoa baada ya talaka.

Wakati wa mwenendo wa shauri la talaka Mahakamani wife aliniomba kikao kupitia wakili wake, mimi sikua na wakili kwenye kesi hiyo, sikuona sababu ya kupoteza pesa zangu, katika kikao hicho waliniomba nikubali talaka mahakamani ili tumalize hiyo kesi Mara moja in return mteja wake hatadai kugawana Mali.

Maana alitaka kufunga ndoa haraka hivyo talaka ndo ilikua kikwazo. Nikakubali mapendekezo yao tarehe ya kesi ilipofika nikaondoa pingamizi la kuzuia hiyo talaka na tukamwambia hakimu tumekubaliana nje ya mahakama hivyo makubaliano ndio yawe hukumu yake.

Katika barua yangu kwenda kwa hakimu sikuandika kwamba naondoa pingamizi kwa kuwa mke wangu kakubali kutodai Mali, Bali nilisema ni kwa sababu nimeona mwanamke hanipendi tena hivyo siwezi kulazimisha mapenzi.

Hakimu akatoa rasmi talaka mwezi februari last year, watoto waliamriwa kubaki na mimi, maana wife aliweka wazi tu kwamba anataka kuolewa na mtu mwingine. Watoto wetu ni wawili, wapo standard six ni mapacha, tuliwapata kabla hatujafunga ndoa kanisani.Contrary to our agreement, miezi sita baada ya talaka kutoka.

Mke wangu akanigeuka na kufungua kesi mpya ya kudai kugawana Mali mahakamani, nilitaharuki sana na kuhaha kumtafuta ili kujua hii samasi niliyoletewa kutoka Mahakamani ni yangu kweli au imekosewa, akawa ananikwepa hakutaka kabisa kuonana na mimi tukawa tunakutania Mahakamani kila kesi ilipotajwa, na hata wakili wake akawa ananikimbia.

Nikamtumia sms kwanini anafanya hivi akanijibu kuwa anataka nyumba iuzwe tuganawane pesa. Usiku nikawaza sana ndani, nikawaambia watoto, ninaingia kwenye mapambano makubwa na mama yenu na sijui vita hii itaisha lini ila mwombeni sana Mungu atuvushe salama kwenye tufani hii na tushinde, ingawa ni watoto wa darasa la sita ila walinielewa.

Kesho yake nikaamkia shirika analofanyia kazi mke wangu na kuomba kuonana na Mkurugenzi wa utumishi nikapekekwa nikaonana nae. Nikamwambia """ bosi mimi ni whistle blower, ni msamaria mwema ninaeipenda nchi hii.

Nina taarifa nyeti kuhusu mfanyakazi wenu, nikataja jina la mke wangu la kazini, kwamba anatumia cheti cha mtu mwingine ambae ni marehemu aliefariki mwaka 2004, nendeni vizazi na vifo mtalikuta jina la mtu huyo, na pia taasisi zifuatazo mtalikuta jina hilo nikazitaja taasisi hizo. Nikamtajia na majina yake halisi, anasema wataifanyia kazi taarifa hiyo

Haukupita mwezi akasimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma za kughushi vyeti, alilia kama mtoto mdogo alijua amekwisha maana ishu nzima ni ya kweli. Miezi mitatu mbele akafutwa kazi rasmi na shirika hilo kubwa kabisa Tanzania linalosifika kwa kulipa vizuri staff wake 

Yote Tisa, kumi takukuru wakampandisha kizimbani kwa tuhuma hizo zenye ushahidi wa wazi na wa moja kwa moja, bado anahangahika na kesi hiyo inayomwendea kombo.Amekonda kupita kiasi, na yule bwana mdogo alietaka kumuoa bomani kakimbia ndoa haipo tena, maana inasemekana dogo alifuata pesa, sasa mwanamke kawa juu ya mawe janki kakimbia, hali yake inasikitisha.Kesi ya kugawana Mali huenda ikafutwa maana mhusika haendi tena na hana tena hela za kulipa wakili hivyo wakili kajitoa 

Wana Jf mwanamke huyu alitaka kunimaliza mimi lengo lake nibaki juu ya mawe, ili achukue na watoto akaishi nao pamoja na huyo jamaa yake lakini nime counter attack na hivyo yamemrudia yeye.

Ilifika pahala anakuja Jirani na kwangu na huyo mpenzi wake wanakaa grocery ya mbele ya nyumba yangu na kuwekeana miguu ili wanioneshee nikawa siwajali kabisa, alipoona hiyo sitishiki ndipo akafungua kesi ya kugawana Mali

Hata hivyo kwa uwezo wa Mungu nimeshaliza nyumba nyingine na nimehamia na ya zamani kupangisha. Tangu aliponifungulia hiyo kesi milango ya baraka imefunguka zaidi, hata Mahakama ikisema lolote sina tatizo kabisa, ingawa Nina mashaka sana kama kesi hiyo itaendelea.Nimesikia tetesi kuwa ndugu wanaandaa msafara wa wazee kuja kuzungumza nami sijajua ni kuhusu nini, lakini sikumficha nilimwambia wazi ex wife wangu kwamba ni mimi ndie nilievujisha taarifa zake kazini kwao asitafute mchawi na nikamwambia kwanini nilifanya hivyo.

Nimeona watu wengi Jf wakitoa mikasa yao ambayo ni mikubwa kuzidi huu wangu nilikua mualikwa (visitor) humu ndani sasa nimeamua kuwaandikeni yangu mwenyewe, kama kuna pahala nimekosea Basi tusameheane, yote ni maisha tu yanapita

Some people have to learn through the hard way

Sometimes the hard way is the only way out

Thanx

Post a Comment

 
Top