Watu 9 wa Familia Moja Wamefariki Buguruni Malapa kwa Ajali ya Moto

Watu 9 wa Familia Moja jijini Dar wamefariki siku ya Jana baada ya Ajali ya Moto kutokea nyumbani kwao.Waliofariki ni pamoja na Bibi akiwa na watoto watatu wa kike na wajukuu watano waliokuwa wanaishi kwenye nyumba hiyo wote wameteketea kwa moto.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Baba wa familia hiyo amenusurika kwa kuwa hakuwepo nyumbani, na kwamba alirejea baada ya kupigiwa simu na majirani kuelezwa kuzuka kwa moto huo ambao chanzo chake kinaelezwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

Aidha, mashuhuda wanasema walishtuka usingizini saa tisa usiku baada ya kusikia kelele za kuomba msaada toka kwa wanafamilia hao ingawa juhudi zotye hazikuzaa matunda kutokana na geti la nyumba hiyo kushika moto na kuwafanya watu waliokuwa wanajaribu kuwaokoa kushindwa kutoa msaada.

Wanafamilia hao wamekutwa wamekufa kwenye chumba kimoja hali inayoashiria kuwa wakiwa katika harakati za kujiokoa walijikusanya sehemu moja hadi mauti ilipowakuta.


Watu 9 wa Familia Moja Wamefariki Buguruni Malapa kwa Ajali ya Moto

Post a Comment

 
Top