Aliyekuwa Mgombea Mbunge katika Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Kalama Masoud ‘Kalapina’ ameibuka na kupinga matokeo akidai atakwenda mahakamani.

Akizungumza na wanahabari leo Makao Makuu ya chama hicho Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kalapina amesema matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa chama cha wananchi CUF ambaye alikuwa anaungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, Abdul Mtulia yalikuwa yamesheheni dosari kubwa.


Amesema katika kata 19 zilizopo katika Jimbo la Kinondoni, mawakala wake walitishiwa na kulazimika kuacha kusimamia vituo walivyokuwa wamepangiwa.Kalapina alitaja baadhi ya maeneo aliyodai mawakala wake walitishiwa na baadae kuamua kuondoka kuwa ni kata za kijitonyama,Tandale, Ndugumbi pamoja na Kigogo.

Alieleza kuwa baada ya kubaini matatizo yote hayo alilazimika kugomea kusaini karatasi ya wagombea ubunge, akiongeza kuwa hatua iliyobaki kwa sasa ni kwenda kufungua kesi mahakamani.“Natarajia kwenda mahakamani kutaka haki, kwa hiyo Jumatatu au Jumanne ijayo nakwenda kufungua kesi,” alisema kalapina.

Post a Comment

 
Top