Kundi  la muziki nchini Kenya linalofanya vizuri sana Africa Mashariki linalojulikana kama  Sauti Sol linatarajia kusafiri kuelekea jijini Lagos nchini Nigeria kuipeperusha bendera ya taifa  la Kenya katika tamasha linalojulikana kama  Inaugral Viewers’ Choice Awards litakalofanyika jumamosi hii nchini Nigeria.

Sherehe hizo zitasindiikizwa na magwiji wa muziki barani Afrika kama  Femi Kuti, Tiwa Savage, Chidinma na wengineo wengi.

Aidha Sauti Sol watapata nafasi ya kujumuika na nyota wengine wa filamu nchini Nigeria kama vile Chinedu Ikedieze, Genevieve Nnaji, Majid Michel, Omotola Jalade-Ekeinde, Rita Dominic na wengineo kibao watakokuwa wakishiriki katika utoaji wa tuzo hizo

Post a Comment

 
Top