Msanii wa bongo flevaLord eyes ambaye siku za hivi karibuni alikabiliwa na kesi ya kuiba vifaa vya gari,sasa habar zilizo tufikia ni kwamba yeye pamoja na wakili wake waliamua kuweka wazi juu ya kesi inayomuanda hivi sasa.Wakili huyu anayekwenda kwa jina la Peter Kibatala alisema kwamba kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiyo mhusika wa kuiba vifaa hivyo lakini sasa hivi wanaachia kwanza Mahakama ndiyo itakayo chukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.Lakini hapo hapo tuliweza kusikia ujumbe kutoka kwa weusi walizungumza na kusema kwamba tukio kama ili limewaathiri pale wanapokutana na watu mbalimbali na kusikia story za watu kusema kwamba wote watakuwa wanahusika katka kesi hiyo wakati ni story ambazo sio za kweli.Baada ya hapo tuliweza pia kusikia ujumbe kutoka kwa Lord Eyez mwenyewe aliweza kuzungumza kusema kwamba mahakama ndiyo itaamua kuchukua sheria kwamba alihusika au ajahusika katika tukio kama hilo la kuiba vifaa vya gari,ambayo kesi hiyo inatarajia kusomwa Mahakama ya Mwanzo siku ya tarehe 13,14 na 15 mwezi huuhapa jijini Dar es Salaam lakini pia alimalizia kwa kusema japokuwa kwa sasa hivi yupo kitaani huku akisikilizia Mahakama imeamuaje kwa hiyo anachotaka kukifanya ni anataka kudondosha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya suprise kwa mashabiki wake katika industries hii ya muziki wa Bongo Fleva.
Post a Comment