Baada ya msanii Steve RnB kutunga wimbo unaofnaya vizuri sana kwenye media mbalimbali unaojulikana kama Jambo Jambo sasa wasanii wengine watatu wameamua kujaribu bahati zao kwa kutumia beat hiyo ya riddim kutoka Jamaica kwa kufanya nyimbo  zao ila beat likiwa lile lile la riddim. Wasanii hao ni pamoja na  Pestman wa Mwanza aliyefanya wimbo uitwao Mi Beautiful, producer Man Walter wa Combination Sound aliyefanya wimbo uitwao Nawaogopa na Lil Ghetto na Baby J waliorekodi wimbo uitwao Mimi na Wewe . Zisikilize hapa kwa pamoja


Post a Comment

 
Top