Katika hali isiyo kuwa ya kawaida msanii wa filamu na
muziki Bongo, Baby Joseph Madaha hivi karibuni alinaswa nyumbani kwa kigogo
anayetoka na Wema anayejulikana kwa jina Clement.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoomba hifadhi ya jina lake,
tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo staa huyo wa filamu na muziki
alionekana akiingia kwa usafiri wa teksi nyumbani kwa kigogo huyo anayeishi
maeneo ya Mwananyamala-Gereji, Dar.
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya sosi huyo, mapaparazi
wetu walimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa jambo hilo.
“Kweli nilikwenda hapo (kwa Clement), mimi sijui kama
niliyeenda kuonana naye ni bwana wa Wema kwa sababu sijawahi kumuona naye na nilimfuata kwa ajili ya
kuzungumza mambo ya kikazi,” alisema Baby Madaha.
Source Global publisher
Post a Comment