Watu wanne washikiriwa na jeshi la polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na ATM card 150 za Benki ya NMB na rist ya majina na namba za siri za kadi hizo usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kuchukua pesa kiasi cha TSH 20,543,200/=
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman Leo amebainisha  hadharani majina ya watu wanne wanaohusishwa na wizi kwa kutumia kadi za  ATM Mkoani humo.Akizungumza na vyombo vya habari jijini Mbeya kamanda Athumani amewataja watuhumiwa hao pamoja na   Jumanne Magere mwenye umri wa miaka 29 mfanyabiashara wa duka mkazi wa Mlowo wilayani Mbozi.Aidha amesema mtuhumiwa wa pili niJuma Kabyelo mwenye umri wa miaka 20 mfanyabiashara wa duka eneo la Msasani  huko Tukuyu,watatu ni Joseph Sospeter mwenye umri wa miaka 20 mkulima na mkazi wa Msasani Tukuyu na wanne ni Miraj mwenye umri wa miaka 34 mfanyabiashara wa Duka Msasani huko Tukuyu ambao wote wamekutwa na kadi 150 za ATM za watu mbalimbali wakiwemo watumishi wa serikali ambapo tayari walikuwa wameshatoa kiasi cha shilingi milioni 20 Laki tano na elfu 43 kutoka mashine ya ATM.

Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa Jumanne Magele alikiri kuwashirikisha watuhumiwa wenzake na kufanikiwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kwamba kadi hizo ni mali za wateja wake ambao wengi ni wa Wilaya ya Mbozi waliokopa bidhaa mbalimbali kwenye duka lake analo uza bidhaa zinazotumia umeme zikiwemo Tv,Radio pamoja na Vyerehani,Magodoro na baiskeli na kwamba wateja wake ndio waliompa kadi hizo pamoja na namba zao za siri[PASSWORD]iliaweze kukata deni analowadai na kuwapatia kiasi cha fedha zinazosalia.Kufuatia tukio hilo watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa katika kituo cha Polisi Tukuyu Rungwe wakati ufuatiliaji ukiendelea kufanyika kwa wamiliki wa kadi hizo za ATM.

Ufuatiliaji unaofanywa pia unalengo la kubaini kama kuna ukopeshaji wa fedha taslimu unaohitaji malipo ya Riba hiyo ili sheria ziweze kufuatwa.Hadi sasa katika uchunguzi haujabaini wizi wa moja kwa moja uliofanywa na watuhumiwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya Habari wala hakuna taarifa ya mtu kuibiwa kwenye  akaunti yake.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Kamishna Msaidizi Diwani Athuman Anatoa wito kwa jamii kuwa makini sana na Transaction zinazohusu Akaunti zao kutokana na malalamiko kadhaa yaliyofikishwa kwenye vituo mbalimbali vya polisi lakini wakiyafuatilia wanabaini kuwa chanzo ni utoaji holela wa namba za siri na Mwenye akaunti.

Post a Comment

 
Top