Filamu mpya ya Jack Zollo - My Life in Crime, kutoka huko
nchini Kenya, imepangwa kuanza kufanyika mwezi wa 9, na kitu kikubwa
kinachowapa watu wengi msukumo, ni bajeti yake ya shilingi milioni 35 za Kenya
ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 600 za Kitanzania kuitengeneza.
Filamu hii itabeba nyota kama vile Melvin Alusa Ainea
Ojiambo, Lenana Kariba, Jeff Koinange na pia star wa filamu wa Naijeria Jim
Iyke atapewa mashavu ndani yake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Filamu hii itafanyika kwa
sehemu huko Mombasa na pia Nairobi ambapo katika sehemu ya maandalizi pia, Jim
Iyke anatarajiwa kutua mwezi mmoja kabla ya shughuli nzima kuanza ili kuanza
kujiweka sawa na mazingira.
Post a Comment