Jana tarehe 29 APRIL 2013 Masai Nyotambofu kutoka kundi la VITUKO SHOW Lenye makaazi yake jijini Dar Es Salaam Ambalo kwa sasa limeweka kambi jijini Tanga kwa takribani mwaka mmoja, Jana msanii huyo alitembelea maeneo ya HALE
nje kidogo ya mji, Safari hii ilikua ni mualiko Rafiki zake wa kimasai
walionyesha kumpenda sana kwa anachokifanya katika utendaji wa taalima
yake ya uchekeshaji, Wamasai walirahi sana alivyotimiza ahadi ya kufika
maeneo hayo. Walimzawadia mavazi hatimaye akayavaa palepale na kupiga
nao picha kama kawaida. Mbali na hivyo hawakuishia hapo walimpa mualiko
mwingine Kijijini kwao morogoro mwenyezi mungu akijaalia mwezi wa sita Masai Nyotambofu Anatakiwa kutia tim masaini maana wengi wana hamu ya kumuona laivu bila chenga. Safari ya Nyotambofu huko HALE ilikua safi sana na mapokezi mazuri mashabiki wengi walipenda sana shangwe za mapokezi hayo. |
Post a Comment