Kampuni ya ndege ambayo inatoa huduma za usafiri Tanzania ya fastjet imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa watanzania katika hali isiyo kuwa ya kawaida nauli ya mwanza ya basi inafanana na ya ndege.
Usafiri wa basi kwenda Mwanza, nauli ni kati ya shilingi 45,000 mpaka 60,000. Fast Jet yenyewe inatoza nauli ya chini kabisa shilingi 43,000, yaani usafiri shilingi 32,000 na kodi shilingi 11,000, jumla shilingi 43,000.
Vilevile unapopanda Fast Jet, haikulazimu kuingia gharama za ziada kwa ajili ya matumizi ya njiani. Kati ya dakika 45 na 60, unakuwa umeshafika unapokwenda.
Unaposafiri na basi, mbali na kutumia saa nyingi njiani, vilevile itakulazimu kununua chakula kuanzia asubuhi, mchana na wakati mwingine jioni, kwani unakuwa bado hujafika. Kwa kifupi, Fast Jet ni mkombozi wa kila Mtanzania.
Hakuna sababu ya kutumia saa nyingi njiani au wakati mwingine kupitisha zaidi ya siku ukisafiri, eti kwa kukimbia gharama za kusafiri kwa ndege, wakati Fast Jet inakusafirisha kwa bei nafuu kuliko hata ile ambayo ungelipa kwa basi.
Mmoja wa wateja ambaye aliwah kutumia ndege hizo kutoka  JNIA kwenda Kia hakusita kueleza kueleza usafiri wa fast jet ulivyo  “Fast Jet ni nafuu sana. Mimi na mtoto wangu tumeweza kusafiri kwenda na kurudi, Kilimanjaro – Dar kwa shilingi 282,000. Unadhani kama ingekuwa ni kwenye makampuni mengine hali ingekuwaje? Nafurahia bei na huduma za Fast Jet.”

Mkuu wa Oparesheni wa Fast Jet, Kia, Robert Kessy alisema Nashauri abiria wawe wanajitahidi kufanya booking mapema ili wapate bei ya chini kabisa ambayo ni shilingi 43,000. Wanapochelewa ndiyo hukutana na bei za juu. Kwa kawaida bei zetu zinaanzia shilingi 43,000 mpaka shilingi 300,000.”

Post a Comment

 
Top