Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge
jijini Dar mishale ya saa 10 usiku ambapo mwanaume mmoja mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo
almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Neema
Samson, mkazi wa Buguruni.
Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume
huyo ambaye ni mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya
mapenzi lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama
wanavyokubaliana.
“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi
na kama hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka
buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa
hasira.
Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na
kuwashuhudia wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia
simu yake aina ya Nokia.
Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa
uwezo wake wote kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida
Joseph akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti,
alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema.
Wawili hao waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema
waliposhirikiana kuwabeba kisha kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo
cha polisi....
Post a Comment