tigo verified



Tigo Tanzania imepiga hatua moja nyingine baada ya kuwa Kampuni ya kwanza Tanzania kuwa Verified katika mtandao wa Twitter. Kabla ya hapo ni wanasiasa kama Rais Jakaya Kikwete na January Makamba pamoja na watu maarufu kama Flaviana Matata na Hasheem Thabeet waliokuwa na kialama cha tick mbele ya majina yao twitter.

Unaweza kujiuliza kuwa verified kwani kuna umuhimu gani, alama ya tick unayowekewa mbele ya jina lako ni utambulisho unaofanya ueleweke kwa followers wako kuwa ni wewe na sie mwingine wanaemfahamu. Alama hii hupewa watu maarufu, makampuni, taasisi na wawakilishi ili kuepusha mkanganyiko unaotokana na kuwepo kwa parody account. Mpaka sasa zipo account 50,000 tu zilizokuwa verified dunia nzima.

Nini Faida Yake?

Tuchukulie mfano wa kilichotokea kwa Tanesco baada ya kuibuka ile account ya @TANESCO_ ,  alama ya kuwa verified pekee ndio yenye uwezo wa kutofautisha Tanesco parody account na Tanesco ya ukweli.  Ni wakati sasa kwa wasanii na watu maarufu ambao kila siku wamekuwa wakilalamika watu kutumia majina yao kuwaibia mashabiki wao kupitia mitandao ya kijamii  kufuata mfano wa Tigo.

Post a Comment

 
Top