Naibu Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amewatoa nje ya bunge wabunge
watano ya Bunge kwa muda wa siku tano akiwamo Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni Tundu Lissu kwa kosa la utovu wa nidhamu na kuanzisha
majibizano bungeni kitendo kinachokiuka kanuni na taritibu za bunge.
Pia ni pamoja na mbunge wa Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI, Mbunge wa Arusha Mjini
GODBLES LEMA, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA, Mbunge wa
Nyamagana EZEKIA WENJE na Mbunge wa Ilemela HIGHNES KIWIA hawa wote walikuwa
wanawazuia askari kumtoa Mh Tundu Lissu bunge leo
Awali kabla ya kikao cha bunge Mbunge wa Iramba Magharibi
Mwigulu Nchemba ndiye aliyekuwa akichangia Bajeti ya Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma.
Mbunge wa Longido Lekule Laizer ni kama ametabiri kutokea
kwa jambo hilo kabla kwani wakati anachangia amepinga vitendo vya vurugu
bungeni hali iliyopelekea kuwakumbuka wabunge wa zamani.
Post a Comment